Si sawa wala si haki kuwabebesha wananchi bei kubwa ya bidhaa kwa sababu tu shirika limejiruhusu kuingia gharama kubwa zaidi kuliko inavyolazimu. Wala siyo sawa au haki kwa Watanzania kukosa kupata ziada katika mashirika ya umma ya uzalishaji mali au ya kibiashara kwa sababu tu mashirika haya yamejiruhusu kuendeshwa kwa njia za gharama zisizo za lazima