WANASEMA mimi ni Mnyarwanda. Hawana ushahidi wa kulithibitisha hilo. Lakini hata kama ni kweli mimi ni Mnyarwanda, ni Mganda gani asilia ambaye ameiendeleza Uganda kushinda mimi ‘wa kuja’ nilivyofanya? Hizi ni siasa muflisi, hawana hoja hao wanaodai kwetu ni Rwanda